Dodoma Jiji vs AZAM FC

vs

Recap

AZAM FC YAPANDA KILELENI LIGI KUU

Ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji usiku huu, umeipaisha Azam FC hadi kileleni mea msimamo wa ligi kuu ya NBC msimu wa 2024/25.

Mabao mawili ya Nassor Saadun katika kila kipindi pamoja na lile la mkwaju wa adhabu kubwa la Feisal Salum mwishoni mea kipindi cha kwanza, yalitosha kuipatia Azam FC ushindi wa kishindo dimbani Jamhuri Dodoma.

Azam FC iliyoingia mwenye michezo huu kikwa na alama 27, sasa inafikisha alama 30 na kuishusha Simba iliyokuwa kileleni na alama 28. Huu ni ushindi wa saba mfululizo kwa vijana wa kocha Rachid Taoussi kutoka Morocco, ambao walianza msimu kwa kusuasua chini ya kocha Youssouph Dabo kutoka Senegal.

Lakini hata hivyo, wenyeji Dodoma Jiji ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao baada ya Yannick Bangala kujifunga mnamo dakika ya 8 akibabatizwa na majaro ya Idd Kipagwile.

Bao hilo halikudumu kwani dakika nne baadaye Nassor Saadun akipokea pasi safi ya Feisal Salum, alipiga shuti la chini chini la nje ya 18 lililotinga kimiani na kuisawazishia Azam FC mamo dakika ya 11.

Azam FC wakacharuka na kupeleka mashambulizi mazito langoni mwa Dodoma Jiji na secunde chachi kabla ya mapumziko, Idd Nado aliangushwa ndani ya enero la habari na kipa wa Dodoma Jiji, Allen Ngeleja, na kuwa penati.

Feisal Salum akaipigia kwa ufundi penati hiyo na kuiweka mbele Azam FC hadi mapumziko.

Dakika ya 60 Saadun akafunga bao la pili kwake na la tatu kwa Azam FC na kuiweka mechi katika mazingira salama upande wao. Bao hilo lilitokana na uwanja wa Gibril Sillah kuvunja mtego wa kuotea na muleta papatu papatu lango kwa Dodoma na Saadun kuvamia na kufunga.

Azam FC

Mohamed Mustafa, Lusajo Mwaikenda, Pascal Msindo, Yannick Bangala, Yoro Diaby, Idd Nado, James Akaminko, Adolf Mtasingwa, Gibril Sillah, Feisal Salum, idd Nado, Nassor Saadun

Dodoma Jiji

Ngeleka Alain, Augustino Samson,  Salmin Hoża, Zidane Sereri, Dissan Galiwango, Mwana Kibuta, Joash Onyango, Dickson Mhilu, Idd Kipagwile, Emotan Eba, Paul Peter.

Video

Details

Date Time League Season
December 1, 2024 4:00 pm NBC Premier League 2024

Results

ClubGoalsOutcome
Dodoma Jiji1Loss
AZAM FC3Win
Goals
0
0
Assists
0
0
Yellow Cards
0
0
Red Cards
0
0