Recap
AZAM FC YAJIPIGIA KAGERA SUGAR
Bao pekee lililotokana na mkwaju wa penalti lililofungwa na kiungo Feisal Salum Abdallah dakika ya 56 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dimbani Azam Complex.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 11 na kupanda nafasi ya pili ikiwazidi tu wastani wa mabao mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi moja mkononi.
Kwa upande wao Kagera Sugar baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao nane za mechi 11 pia nafasi ya 14.
Azam FC
Mohamed Mustafa, Lusajo Mwaikenda, Pascal Msindo, Yoro Diaby, Yeison Fuentes, James Akaminko, Ever Meza, Idd Nado, Gibril Sillah, Feisal Salum, Nassor Saadun.
Kagera Sugar
Ramadan Chalamanda, David Luhende, Samwel Onditi, Abdallah Mfuko, Geofrey Manyasi, Richardson Ngondya, Mohamed Mussa, Eric Mwijage, Omary Chibada, Kassim Feka, Hijjah Shamte.
Details
Date | Time | League | Season |
---|---|---|---|
November 23, 2024 | 7:00 pm | NBC Premier League | 2024 |
Results
Club | Goals | Outcome |
---|---|---|
AZAM FC | 1 | Win |
Kagera Sugar | 0 | Loss |
0 |
|
0 |
0 |
|
0 |
0 |
|
0 |
0 |
|
0 |