ASHRAF KIBEKU ASAINI MIAKA MITANO

Beki chipukizi kutoka akademi mwenye uwezo mkubwa wa kupanda na kushuka, Ashraf Kibeku, amesaini miaka mitano na timu kubwa ya Azam FC na kujifunga kuwa Chamazi hadi mwaka 2030.

Ashraf alijiunga na akademi ya Azam FC mwaka 2018 akianzia timu ya chini ya miaka 13, na kupanda kidogo kidogo hadi sasa mesaini timu kubwa.

Safari yake ya kupanda hadi timu kubwa ilikuwa kama ifuatavyo

Under 13: 2018

Under 15: 2019
Under 17: 2021

Under 20: 2022

Mashindano

TFF U-17 Premier League 2021(18 matches 7 goals with 15 assists including 5 assists in one match)

TFF U-17 Premier League 2022 (2 matches- suffered long-time injury)

Under 20: Azam FC
-East Africa Chipukizi Cup Arusha – 2021(All 7 matches with 2 assists)

– East Africa Chipukizi Cup Arusha – 2022(All 7 matches with 2 goals and 4 assists) Best player of the tournament.

Timu kubwa

Ashraf alianza kuchezea timu kubwa mwaka 2023 pale alipojumuishwa na kocha Kali Ongala kwenye kikosi kilichoenda kwenye Kombe la Mapinduzi Cup 2023.

Japo hakupata nafasi kwenye mashindano hayo, lakini alicheza mechi mbili za kirafiki; dhidi ya Mafunzo ambayo alitoa pasi ya bao, na chidi ya Polisi ambayo alifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.

Ashraf Kibeku alizaliwa mkoani Morogoro, Disemba 20, 2006.