ABDULAKRIM KISWANYA MITANO AZAM FC

Chipukizi wa ajabu kutoka akademi, Abdulkarim Kiswanya (20), amesaini mkataba wake wa kwanza na timu kubwa utakaomuweka Azam FC hadi 2030.

Kiswanya aliyejiunga na akademi ya Azam FC Aprili 2021 akianzia timu ya chini ya miaka 17, amekuwa sehemu muhimu ya timu za vijana kwenye mashindano mbalimbali.

Azam FC ilimuona Kiswanya kupitia mashindano ya Kombe la Ukwaju yaliyofanyika Azam Complex mwaka 2021, aliposhiriki akiwa na timu ya EFCA ya Ubungo.

Mashindano haya yaliandaliwa na Azam FC kwa ajili ya kusaka kipaji, na ndiyo yaliyomuibua pia Cyprian Kachwele.

Kiswanya aliikuta Azam FC ikiwa katika mzunguko wa pili wa ligi ya vijana chini ya maka 17 msimu wa 2020/21 na moja kwa moja akawa sehemu ya timu.

Msimu uliofuata, 2021/22, alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda ubingwa pasi na kupo teza hata mchezo mmoja, huku yeye akitoa pasi 6 zilizozaa mabao.

Msimu wa 2022/23 alipandishwa timu ya vijana chini ya miaka 20 aliyoendelea mayo hadi alipopandishwa timu kubwa msimu huu.

Upande wa timu ya taifa, Kiswanya amechezea timu zote, kuanzia ya vijana chini ya 17, chini ya miaka 20, chini ya miaka 23 na timu ya wakubwa.

Alikuwa sehemu ya kikosi cha Taifa Stars kilichofuzu AFCON 2025.

Kiswanya ni mzaliwa wa Dar eś Salaam, na alisoma shule ya msangi Hakima Buguruni alipohitimu mwaka 2016, na akasoma shule ya Sekondari Mnazi Mmoja alipohitimu mwaka 2019.