Tabora United 2-1 AZAM FC

vs

Recap

HAIKUWA SIKU YETU HAPA TABORA

Haikuwa siku zuri kwa Azam FC hapa mjini Tabora lakini zaidi haikuwa siku zuri kwa mlinda lango Mohamed Mustafa, kutoka Sudan. Makosa mawili ya kila kipindi kwa kipa huyo mahiri, yaliifanya Azam FC ipoteze mchezo wa kwanza baada ya kuwa ilishinda mechi saba mfululizo.

Mpira mrefu wa Morice Chukwu uliokana kukesa madhara hadi pale Mohamed Mustafa alipokosea hesabu na kuzidiwa maarifa na Heritier Makambo aliyepiga kichwa na kufunga bao la kwanza mnamo dakika ya 38.

Kipindi cha pili Mohamed Mustafa alifanya kosa lingine lililoipatia Tabora United bao la pili akiuingizj mwenyewe ndani ya nyavu mpira wa maj aro wa Heritier Makambo mnamo dakika ya 68.

Mlinzi raia wa Mali, Mamadou Yoro Diaby, aliifungia bao Azam FC mnamo dakika ya 71 alipomalizia kwa kichwa mpira wa kona kutoka kwa Feisal Salum. Bao hilo likarejesha matumaini lakini hata hivyo Tabora United walisimama imara kulinda ushindi wao hadi mwisho wa mchezo.

Azam FC

Mohamed Mustafa, Lusajo Mwaikenda, Pascal Msindo, Yeison Fuentes, Yoro Diaby, James Akaminko, Gibril Sillah, Adolf Mtasingwa, Nassor Saadun, Feisal Salum, Idd Nado.

Tabora United

Hussein Masalanga, Emmanuel Chigozie, Faria Odongo, Pemba Kingu, Andy Bikoko, Nelson Munganga, Offen Chikola, Ogochukwu Morice, Heritier Makambo, Issah Ngoah, Banele Shikondze.

Video

Details

Date Time League Season
December 13, 2024 4:00 pm NBC Premier League 2024

Ground

Azam Complex
Azam Complex

Results

Club1st Half2nd HalfGoalsOutcome
Tabora United112Win
AZAM FC011Loss
Goals
0
0
Assists
0
0
Yellow Cards
0
0
Red Cards
0
0