Recap
AZAM FC YAVUNJA MWIKO SOKOINE
Kwa mara baada ya miaka zaidi ya mitano, Azam FC imepata ushindi dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mabao mawili ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Idd Nado na Nassor Saadun yaliihakikishia Azam FC ushindi wa kwanza dimbani hapo tangu Januari 20, 2018 iliposhinda 2-0 pia kwa mabao ya vijana wa akademi, Yahya Zayd na Paul Peter.
Katika mchezo wa leo, Azam FC ilipata bao la kwanza dakika ya 12 kupitia Idd Nado aliyepokea pasi ya karibu kutoka kwa Gibril Sillah ambaye aliuwahi mpira uliomshinda kipa wa TZ Prisons, Mussa Meise, kufuatia kross ya Nassor Saadun.
Dakika mola kabla ya mapumziko, Nassor Saadun akafunga bao la pili akiunganisha majaro ya Lusajo Mwaikenda kutokea upande wa kulia wa uwanja.
Mchezo huu pia ulishuhudia beki wa Azam FC, Abdallah Heri ‘Sebo’ akicheza kwa mara ya kwanza tangu alipoumia msimu uliopita katika mchezo wa pili tu wa msimu wa 2023/24 dhidi ya hawa hawa TZ Prisons dimbani Azam Complex.
Sebo aliumia ACL katika michezo wa Agosti 28, 2023 na akafanyiwa mabadiliko wakazi wa mapumziko. Akafanyiwa upasuaji uliomuweka nje kwa mwala mima hadi alipingia kipindi cha pili patika michezo wa leo.
Azam FC
Zuberi Foba, Lusajo Mwaikenda, Pascal Msindo, Yeison Fuentes, Yoro Diaby, James Akaminko, Adolf Mtasingwa, Idd Nado, Gibril Sillah, Feisal Salum. Nassor Saadun.
Details
Date | Time | League | Season |
---|---|---|---|
October 18, 2024 | 4:00 pm | NBC Premier League | 2024 |
Results
Club | Goals | Outcome |
---|---|---|
Tanzania Prison | 0 | Loss |
AZAM FC | 2 | Win |
0 |
|
0 |
0 |
|
0 |
0 |
|
0 |
0 |
|
0 |