Recap
AZAM FC YAUANZA MSIMU KWA SULUHU DHIDI YA JKT TANZANIA
Sare ya bila kufungana imeifanya Azam FC kuanza vibaya msimu mpya wa ligi kuu ya NBC wa 2024/25 dhidi ya JKT Tanzania kenye dimba la Meja Isamuhyo, Mbweni Dar es Salaam.
Kocha Yousuoph Dabo alifanya mabadiliko manne kwenye kikosi kutoka kile kilichoanza dhidi ya APR kwenye ligi ya mabingwa, wiki moja iliyopita. Aliwaacha nje Frank Tiesse na Jhonier Blanco kwenye safu ya ushambuliaji na nafasi zao kuchukuliwa na Idd Nado na Nassor Saadun mtawalia. Pia kwenye safu ya ulinzi alimtoa Cheikh Sidibe na nafasi yake kuchukuliwa na Nathan Chilambo. Na kwenye safu ya kiungo, alimuacha nje James Akaminko na nafasi yake kuchukuliwa na Ever Meza.
Nassor Saadun aliifungia bao Azam FC mnamo dakika ya 28 lakini hata hivyo halikukubaliwa kda sababu alikuwa ameshaotea kabla ya kufunga. Kwa jumla haukuwa mchezo wenye kashikashi nyingi kwa Azam FC hadi zilipoongezwa dakika saba baada ya tisini za kuandika, ndipo ari ya kutafuta ushindi ilipopanda kwa wachezaji, lakini hata hivyo hakuna kilichobadilika hadi mwisho wa mchezo.
Kocha Dabo amesema amesikitishwa na matokeo lakini watarudi kwenye uwanja wa mazoezi kufanya marekebisho ya mapungufu yaliyojitokeza ili kurudi kwenye mstari.
Mchezo ujao ni dhidi ya Pamba Jiji dimbani Azam Complex, Septemba 14.
Azam FC
Mohamed Mustafa, Lusajo Mwaikenda, Nathan Chilambo, Yannick Bangala, Yeison Fuentes, Ever Meza, Adolf Mtasingwa, Idd Nado, Gibril Sillah, Feisal Salum, Nassor Saadun
Details
Date | Time | League | Season |
---|---|---|---|
August 28, 2024 | 4:00 am | NBC Premier League | 2024 |
Results
Club | 1st Half | 2nd Half | Goals | Outcome |
---|---|---|---|---|
JKT Tanzania | 0 | 0 | 0 | Draw |
AZAM FC | 0 | 0 | 0 | Draw |
0 |
|
0 |
0 |
|
0 |
0 |
|
0 |
0 |
|
0 |