AZAM FC 0-0 Pamba Jiji

vs

Recap

RACHID TAOUSSI AANZA KWA SARE SIDIBE AKIONESHWA KADI NYEKUNDU

Timu ya Pamba Jiji kutoka Mwanza imemkaribisha kibabe Rachid Taoussi kama kocha mpya wa Azam FC baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana dimbani Azam Complex.

Taoussi amejiunga na Azam FC mwezi huu akichukua nafasi ya Yousouph Dabo aliyefutwa kazi baada ya sare dhidi ya JKT Tanzania, mwishoni mwa mwezi uliopita.

Kocha huyo raia wa Morocco alianzisha kikosi kisicho na nyota wake kadhaa waliokuwa timu ya taifa wakiongozwa na kinara wao wa mabao msimu uliopita, Feisal Salum.

Azam FC ilipoteza nafasi nyingi za wazi na kuufanya mchezo uende mapumziko matokeo yakiwa bila bila. Kipindi cha pili, mlinzi wa kushoto wa Azam FC, Cheikh Sidibe alioneshwa kadi nyekundu baada ya kuoneshwa kadi mbili za njano.

Kupungua kwa Azam FC kukawapa nafasi Pamba kushambulia zaidi na almanusura wapate bao mnamo dakika ya mwisho ya mchezo baada ya Ben Nakibinge kufunga bao lakini lilikataliwa kwa sababu filimbi ilishapigwa kabla hajaupiga mpira.

Mechi imago itakuwa Septemba 19 didi ya KMC mwenye uwanja wa KMC Complex Mwenge.

Azam FC

Zuberi Foba, Nathan Chilambo, Cheikh Sidibe, Yoro Diaby, Yeison Fuentes, Ever Meza, James Akaminko, Gibril Sillah, Jhonier Blanco, Nassor Saadun, Idd Nado

 

Details

Date Time League Season
September 13, 2024 7:00 pm NBC Premier League 2024

Ground

Azam Complex
Azam Complex

Results

Club1st Half2nd HalfGoalsOutcome
AZAM FC000Draw
Pamba Jiji000Draw
Goals
0
0
Assists
0
0
Yellow Cards
0
0
Red Cards
0
0