Recap
AMAAN HAKUNA AMANI
Azam FC imepoteza michezo wake wa kwanza msimu huu kwa kufungwa 2-0 dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar.Hata hivyo, huu ulikuwa mmoja wa michezo iliyosimamiwa kibaya na waamuzi kutokana na kupitisha sheria nyingi za soka.
Mabao yote ya Simba yalitokana na wafungaji kuotea wazi kabisa lakini waamuzi hawakuchukua hatua.
Feisal Salum alikaribia kuifungia bao Azam FC mapeia kipindi cha kwanza lakini shuti lake kali la mguu wa kushoto likagonga mwamba na kutoa nje.
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Mashujaa, Septemba 29.
Azam FC
Mustafa Mohamed, Lusajo Mwaikenda, Pascal Msindo, Yoro Diaby, Fuentes Mendoza, James Akaminko, Idd Nado, Gibril Sillah, Nassor Saadun, Feisal Salum.