Kufuatia kipigo cha kushtukiza cha 2-1 kutoka Namungo FC kwenye uwanja wa nyumbani, kocha Kali Ongala amesema ameumizwa na matokeo lakini zaidi kiwango cha chini cha timu nzima kwa ujumla. Akiongea na azamfc.com baada ya mchezo huo, kocha Kali amesema kiwango cha kujituma, nidhamu ya kimbinu na kufuata maelekezo vilikuwa chini sana kutoka kwa wachezaji wake.
“Kwa kweli nimeumizwa sana na haya matokeo. Leo sitolala kabisa kwa sababu tumepoteza mchezo lack of commitment and tactical discipline ya wachezaji wetu. Mechi kama hizi ndizo zinazotofautisha timu ya ubingwa na timu ya daraja la kati. Mechi dhidi ya Simba au Yanga zina-motivate (hamasisha) wachezaji automatically(zenyewe) lakini mechi kama hizi wachezaji wanatakiwa kuji-motivate wenyewe.”
Kali alikuwa akirejea kiwango cha wachezaji wake kwenye mchezo uliopita wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports dhidi ya Simba ambapo wachezaji walionesha uwezo wa juu.
“Timu ya ubingwa hudhihirisha kwenye mechi kubwa lakini zaidi mechi ndogo kama hizi kwa sababu hizi ndizo ziko nyingi. Wachezaji wanapaswa waelewe kwamba kilicho muhimu ni alama tatu, ziwe kutoka timu kubwa au ndogo.”
Katika mchezo huo, Azam FC ilikuwa ya kwanza kupata bao baada ya mlinzi wa Namungo Partene Counou kujifunga wakati akijaribu kuokoa krosi ya Idris Mbombo, mnamo dakika ya 19.
Namungo wakasawazisha dakika ya 25 kupitia Hassan Kabunda aliyeachia shuti kali la mguu wa kushoto baada ya kupokea pasi ya Jacob Massawe. Hadi mapumziko matokeo yalikuwa 1-1.
Kipindi chja pili Namungo wakapata bao la pili lililofungwa na Shiza Kichuya mnamo dakika ya 55 akipokea pasi ya Frank Domayo.
Azam FC ilipambana kupata bao la kusawazisha lakini haikuwa bahati.
Hadi mwisho Namungo wakashinda 2-1 na kuwafanya kupata ushindi wao wa kwanza Azam Complex.
Azam FC
Abdullahi Iddrisu, Lusajo Mwaikenda/Nadhan Chilambo (89′), Pascal Msindo, Abdallah Heri, Daniel Amoah, Isah Ndala/Kenneth Muguna(65′), Ayub Lyanga/Prince Dube (65′), James Akaminko, Idris Mbombo, Yahya Zayd/Abdul Hamis Sopu (57′) Kipre Jr./Iddy Nado (57′).