wachezaji watatu wa Azam FC walioanza na kumaliza mchezo wa nusu fainali ya Kombe la shirikisho la Azam Sports dhidi ya Simba, Abdallah Heri ‘Sebo’, Abdul Hamis Suleiman Sopu na Sospeter Bajana, wamesema waliufurahia mchezo huo kwa sababu walicheza kwenye mazingira waliyoyazoea.

Katika vipindi tofauti vya maendeleo ya soka lao, wachezaji hawa waliitumikia timu ya Ndanda SC ya Mtwara ambayo uwanja wake wa nyumbani ndiyo uliotumika kwenye nusu fainali, Nangwanda Sijaona.

Wakiongea na azamfc.com baada ya mchezo, watatu hao wamesema wamefurahi sana kurudi katika uwanja ambao umechangia maendeleo yao ya soka. Wanasema Ndanda iliwapa nafasi ya kuendeleza vipaji vgya na heshima yao kiwa klabu hiyo ni kubwa ikiwemo kulinda heshima ya uwanja wa Nangwanda, kamam ilivyokuwa jana.

Sospeter Bajana aliichezea Ndanda nusu msimu wa 2015/16 alipoenda kwa mkopo dirisha dogo la Disemba 2015. Bajana akiwa na miaka 19 wakati huo, alitoka kupandishwa timu kubwa misimu miwili iliyopita baada ya kuhitimu akademi, lakini nafasi yake ilikuwa ndogo kwenye timu na ndipo akatolewa kwa mkopo ili apate uzoefu. Ndanda wanamkumbuka kwa mabao yake muhimu, lililowapa ushindi wa ugenini dhid ya Coastal Union Februari, 02, 2016 na lile lililowapa sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar, Februari 7, 2016.

Abdallah Heri Sebo Ndanda FC kwa mkopo akitokea.Azam FC msimu wa 2016/17. Sebo ambaye alijiunga na Azam FC msimu wa 2014/15 akitokea Zimamoto ya Zanzibar na kuwemo kwenye kikosi kilichoandika historia kwa kushinda Kombe la Kagame bila kuruhusu hata bao moja mwaka 2015 chini ya kocha Stewart John Hall, alipoteza namba baada ya ujio wa kocha Zeben Hernandez kutoka Hispania mwaka 2016. Ndipo akaenda Ndanda kwa mkopo kupata uzoefu, Baada ya hapo akarudi na kudumu hadi sasa.

Abdul Hamis Suleimani Sopu alicheza Ndanda SC kwa mismu miwili, 2017/18 baada ya kurejea kutoka fainali za AFCON za vijana chini ya miaka 17, mwaka 2017 zilzofanyika Gabon. Akacheza hapo msimu mmoja na baadaye kujiunga na akademi ya Simba lakini hakudumu sana na akaamua kruudi tena Ndanda alikocheza tena msimu wa na 2018/19 kisha kutimkia Coastal Union na mwaka 2022 kujiiunga na Azam FC.

Uzoefu walioupata wakiwa kwenye klabu Ndanda wakicheza uwanja wa Nangwanda ndiyo uliokuwa na msaada mkubwa kwao katika mchezo huu. Mashabiki wa klabu ya Ndanda wanawakumbuka sana na baadhi yao waliwashangilia kwenye mchezo wa nusu fainali.