Kikosi cha Azam FC kimemaliza mazoezi yake ya mwisho kabla ya mchezo wa kesho dhidi ya JKU ya zanzibar. Mchezo huo wa kirafiki ni maalumu kwa ajili ya kupima maendeleo ya kiufundi kuelekea mchezo wa robo fainali dhidi ya Mtibwa Sugar, Aprili 3 mwaka huu.

Kocha Kali Ongalla amesema mchezo huo ni muhimu kwa ajili ya kuangalia namna wachezaji watavyokajibu mapigo (reaction) baada ya matokeo yasiyoridhisha ya hivi karibuni hasa katika viwanja vya ugenini. Kali ameongeza kwamba anajua hawajali kama JKU ni mpinzani wa namna gani bali wanataka kuona namna wachezaji wamefuta jinamizi la kucheza chini ya kiwango katika michezo hiyo.

Mchezo huo utafanyika kesho, Machi 22, saa moja kamili usiku kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.