TUNAPENDA kuufahamisha umma kuwa, tumemtoa kwa mkopo wa miezi sita kiungo wetu mshambuliaji, Tape Edinho, kwenda klabu ya Stella Abidjan ya kwao Ivory Coast.
Edinho anaondoka ili kupisha usajili wa kipa wetu mpya, Abdulai Iddrisu, tuliyemsajili kwenye dirisha dogo akitokea Bechem United ya Ghana, ambapo hivi sasa tutakuwa tumetimiza sheria ya kuwa na wachezaji 12 wa kigeni.

Kiungo huyo mshambuliaji, atarejea kwenye kikosi chetu mwishoni mwa msimu huu atakapomaliza muda wa mkopo ndani ya miamba hiyo ya Ivory Coast.
Azam FC tulimsajili Edinho msimu huu akitokea klabu ya ES Bafing ya kwao na kusaini mkataba wa miaka mitatu.