BODI ya klabu ya Azam imesitisha mkataba na Denis Lavagne, kama kocha mkuu, kuanzia leo, Oktoba 22, 2022.

Uamuzi huo ni kwa maslahi mapana ya klabu na mustakabali wa mradi wake wa maendeleo ya kiufundi.

Denis Jean Lavagne, raia wa Ufaransa, alijiunga na Azam FC Septemba 7 mwaka huu akisaini mkataba wa mwaka mmoja uliomtaka aifikishe klabu kwenye angalau hatua ya makundi ya mashindano ya Afrika.

Kwa bahati mbaya mahitaji hayo ya kimkataba hayakufikiwa hivyo bodi ikafikia uamuzi huu.

Kwa sasa timu itakuwa chini Kalimangonga Sam Daniel Ongala na Agrey Moris hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

Bodi inamshukuru Lavagne kwa jitihada zake za kuisaidia klabu yetu na weledi mkubwa aliouonesha alipokuwa nasi.

Aidha inamtakia kila la heri huko aendako.