KIKOSI cha Azam FC kinatarajia kupasha misuli joto kikiivaa JKU ya Zanzibar katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex kesho Jumamosi saa 10.00 jioni.

Mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya kuwaweka kwenye ushindani wachezaji, baada ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara (NBCPL) kuwa kwenye mapumziko.

Wachezaji wa Azam FC wakiwa kwenye maandalizi.

Wakati wa mapumziko, kikosi cha Azam FC kinaendelea na maandalizi makali kuelekea mechi zijazo za ligi, ambapo Novemba 21, kitacheza dhidi ya KMC, mchezo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru saa 10.00 jioni.

Hadi ligi inaelekea mapumzikoni, Azam FC imejikusanyia jumla ya pointi saba ikiwa nafasi ya nane kwenye msimamo baada ya ushindi mechi mbili, sare moja na kupoteza miwili.