KLABU ya Azam imeendesha kozi maalumu ya askari wasimamizi wa viwanja kwenye mechi (stewards), ambayo imefungwa rasmi leo Jumanne kwenye viunga vya Azam Complex.

Kozi hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Afisa Ulinzi na Usalama Viwanjani wa FIFA, ASP Mohamed Manyahe, anayetambulika pia na Serikali, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na la Afrika (CAF).

Afisa Ulinzi na Usalama Viwanjani wa FIFA, ASP Mohamed Manyahe, akiendesha kozi hiyo.

Kozi hiyo ilihusisha maofisa pekee wa ulinzi wa Azam FC, pamoja na wafanyakazi wengine ambao kwa ujumla wanapewa ujuzi huo kwa ajili ya kufanya kazi hiyo kwa uweledi mkubwa.

Katika ufungaji wa kozi hiyo, uongozi wa Azam FC uliwakilishwa na Mkurugenzi wa Mpira wa Azam FC, Dk. Jonas Tiboroha, aliyeambatana na nyota na Meneja wa zamani, Phillip Alando, aliyefunga kozi akimwakilisha Mwenyekiti, Nassor Idrissa ‘Father’.

Wanafunzi wa kozi hiyo wakisikiliza kwa makini

Kozi hiyo inatarajia kuendelea tena kwa hatua ya pili katika siku za usoni, lengo likiwa ni kuwanoa vilivyo askari hao.