BEKI kisiki wa Azam FC, Daniel Amoah, ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili zaidi kuendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex.

Amoah amesaini mkataba huo mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ leo Alhamisi.

Mkataba huo mpya utamfanya Amoah kubakia Azam FC hadi Agosti 2024, ambapo ule wa awali ulikuwa unamalizika utakapoisha msimu huu Julai 31, 2022.

Beki wa kati wa Azam FC, Daniel Amoah, aliposaini mkataba mpya kwenye Ofisi za Mzizima, jijini Dar es Salaam.

Beki huyo raia wa Ghana amekuwa na kiwango kizuri katika eneo la ulinzi la beki wa kati tokea ajiunge na Azam FC Agosti, 2016 akitokea Medeama ya nchini kwao.

Msimu huu amefanikiwa kucheza mechi zote tisa za mashindano za Azam FC, akifanikiwa kufunga bao moja, Azam FC ilipotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Coastal Union.