KLABU ya Azam FC imeajiri makocha wapya wa timu zake za vijana chini ya umri wa miaka 17 (Azam FC U-17) na 20 (Azam FC U-20).

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, amemtambulisha Kocha Mussa Rashid kuwa Kocha Mkuu wa Azam FC U-20.

Kocha mpya wa Azam FC U-20, Mussa Rashid, akisaini mkataba mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’.

Rashid aliyekuwa akiinoa African Sports, anachukua mikoba ya Vivier Bahati, aliyepandishwa kuwa Kocha Msaidizi wa timu kubwa ya Azam FC chini ya George Lwandamina.

Popat pia amemtangaza kocha wa zamani wa Mtibwa Sugar, Gwambina na Malindi, Mohamed Badru, kuwa Kocha Mkuu wa Azam FC U-17.

Kocha mpya wa Azam FC U-17, Mohamed Badru, akisaini mkataba mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’.

Wawili hao wamesaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja, utakaowafanya kuzitumikia timu hizo hadi mwaka 2023.

Aidha Popata, amewakabidhi makocha wote falsafa mpya ya Azam FC, ambayo wanatakiwa kuifuata katika kuwanoa wachezaji wa vikosi hivyo.