JUMLA ya wachezaji 24 wa Klabu bora kabisa nchini ya Azam FC, wamesafiri alfajiri ya leo Jumamosi, tayari kwa mechi mbili za ugenini za ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania.

Azam FC itaanza kufungua pazia la ligi hiyo dhidi ya Coastal Union keshokutwa Jumatatu kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga saa 10.00 jioni, kabla ya kuelekea jijini Moshi, Kilimanjaro kumenyana na Polisi Tanzania Oktoba 02, mwaka huu.

Kocha Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina, mara baada ya mazoezi ya mwisho jana Ijumaa jioni kwenye viunga vya Azam Complex, amechagua kikosi cha wachezaji 24 watakaojiandaa na mechi hizo mbili za kwanza.

Jeshi kamili la Azam FC ambalo litavaana na Coastal Union na Polisi Tanzania.

Kikosi hicho kamili kilichosafiri kinaundwa na;

Makipa

Mathias Kigonya, Ahmed Suleiman Salula, Wilbol Maseke na Zubeir Foba.

Mabeki

Nickolas Wadada, Abdul Omary ‘Hamahama’, Bruce Kangwa, Edward Manyama, Daniel Amoah, Yvan Mballa, Abdallah Kheri Sebbo na Lusajo Mwaikenda.

Viungo

Sospeter Bajana, Paul Katema, Kenneth Muguna, Never Tigere, Tepsie Evance, Frank Domayo ‘Chumvi’, Idd Seleman ‘Nado’, Ayoub Lyanga, Charles Zulu na Ismail Aziz Kader.

Washambuliaji

Idris Mbombo na Rodgers Kola.