AZAM FC tunayofuraha kuwataarifu kuwa, tumeingia mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Idris Mbombo, tuliyemnunua kutoka El Gouna ya Misri.

Mbombo amesaini mkataba huo mbele ya Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’, utakaomfanya kuhudumu ndani ya timu yetu hadi mwaka 2023.

Mshambuliaji, Idris Mbombo (kushoto), akionyesha uzi wa timu yake mpya, akiwa sambamba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’.

Mshambuliaji huyo hatari, aliyewahi kuzichezea kwa mafanikio timu za Nkana, Zesco United, Kabwe Warriors (zote za Zambia), anakuja kuongeza nguvu kwenye safu yetu ya ushambuliaji.

Huo unakuwa usajili wetu wa sita kwenye dirisha hili tukijiandaa na msimu ujao, awali tukiwasajili nyota watatu kutoka Zambia, kiungo mshambuliaji Charles Zulu, kiungo mkabaji Paul Katema, mshambuliaji Rodgers Kola, kiungo mshambuliaji Kenneth Muguna (Kenya) na beki wa kushoto mzawa, Edward Manyama.