MSHAMBULIAJI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Donald Ngoma, leo ameanza rasmi mazoezi ya kuchezea mpira na wenzake.

Ngoma aliyekuwa akifanya mazoezi mepesi kwa kipindi chote kwa takribani wiki sita, amepona majeraha ya kuchanika mtulinga wa kati wa goti lake la mguu wa kulia yaliyokuwa yakimsumbua.

Nyota huyo kutoka Zimbabwe alianza na mazoezi ya viungo ya kawaida kabla ya kuhamia kwenye yale ya kuchezea mpira, ambapo anatarajia kuendelea na programu hiyo hadi atakapokuwa fiti kabisa kwa asilimia 100.