MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, wanatarajia kucheza mechi ya kwanza ya kirafiki kwenye kambi yake nchini Uganda dhidi ya URA, mchezo utakaofanyika Uwanja wa Namboole keshokutwa Ijumaa saa 10.00 jioni.

Azam FC inaendelea na kambi yake ya wiki mbili nchini humo kujiandaa na msimu ujao, ambapo benchi la ufundi limekuwa likiwapa mazoezi kabambe wachezaji wa timu hiyo ili kukindaa vema kikosi hicho.

Mbali na mechi hiyo na URA, kwa mujibu wa programu yake ikiwa nchini humo, Azam FC inatarajia kucheza mechi nyingine tatu za kirafiki dhidi ya Onduparaka, KCCA na Vipers.

Wakati ikifikisha siku ya tatu leo jijini Kampala, Uganda, Azam FC leo Jumatano inatarajia kufanya mazoezi saa 7 mchana kwenye Uwanja wa KCCA uliopo Lugogo, jijini Kampala.