MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kati ya Azam FC na Yanga iliyokuwa ifanyike Jumatatu hii saa 10.00 jioni, sasa imesogezwa mbele kidogo hadi saa 2.00 usiku.

Tayari kikosi cha Azam FC kimeshaanza maandalizi tokea juzi kikijiandaa vilivyo kuelekea mchezo huo wa mwisho wa ligi utakaofanyika Uwanja wa taifa, Dar es Salaam.

Hadi kuelekea mchezo huo wa mwisho wa ligi, timu hizo ziko kwenye vita kali ya kuwania nafasi ya pili, Azam FC ikiwa inaishikilia kwa pointi zake 55 ikiizidi pointi nne Yanga yenye mechi mbili mkononi.