TIMU ya vijana ya Azam FC chini ya umri wa miaka 20 ‘Azam U-20’ imeishushia kipigo kizito cha mabao 15-1 Sweya SC, katika mchezo wa kirafiki uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Azam U-20 inayonolewa na Kocha Mkuu Meja Abdul Mingange, ilifanikiwa kupata mabao sita kwenye kipindi cha kwanza, yaliyofungwa na beki wa kulia Abdul Omary ‘Hama Hama’, kiungo Twaha Hashir na Novatus Dismas, kila mmoja akifunga mara mbili.

Kipindi cha pili Azam U-20 ilijipatia mabao mengine tisa kupitia kwa Richard, Tepsi Evance, Ashraf Said, Said John, Omary Banda, waliofunga moja kila mmoja huku Jamal Abdul na Zackaria Audi wakiingia nyavuni mara mbili kila mmoja.