MSHAMBULIAJI hatari wa timu ya Vijana ya Azam FC ‘Azam U-20’, Andrew Simchimba, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa timu hiyo (Uhai Player Of The Month) mwezi Oktoba-Novemba.

Simchimba ametwaa tuzo hiyo baada ya kufanya vizuri akiwa na timu hiyo, hali iliyopelekea kupandishwa kwenye timu kubwa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba, wiki chache zilizopita wakati Azam FC ikijiandaa kucheza na Njombe Mji.

Mshambuliaji huyo anakuwa mchezaji wa tatu wa timu hiyo ya vijana kubeba tuzo hiyo tokea zilipoanzishwa msimu huu baada ya awali kiungo Twaha Rajab kuitwaa Agosti-Septemba kabla ya mshambuliaji mwingine aliyepandishwa Paul Peter kuinyakua mwezi Septemba-Oktoba.

Tuzo hiyo inadhaminiwa na wadhamini namba mbili wa Azam FC, Maji ya Uhai Drinking Water, ambayo ni tulizo kwa koo lako na safi kabisa kwa kukata vilivyo kiu yako, kikiwa ni kinywaji kutoka Bakhresa Food Products Limited.