KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mama yake mzazi, Wazir Junior, kilichotokea usiku wa kuamkia leo Lushoto mkoani Tanga.

Kutokana na msiba huo mzito kwa familia ya Junior, mshambuliaji huyo wa Azam FC amesafiri asubuhi hii kutoka Njombe, alipokuwepo na kikosi cha timu hiyo kuelekea Lushoto kuhudhuria mazishi.

Uongozi wa Azam FC kwa niaba ya mashabiki na klabu kwa ujumla, unapenda kutoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na familia ya Junior kwa msiba huu mzito, tunawaomba wawe watulivu na Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi katika kipindi hiki kigumu.

Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Raji’un.

#RIPMama