WACHEZAJI wanne wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, wamechaguliwa kujiunga na timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23.

Wachezaji hao walioitwa ni kipa Metacha Mnata, beki Abbas Kapombe (mkopo Ndanda), kiungo Masoud Abdallah na mshambuliaji Yahya Zayd.

Kikosi cha timu hiyo Taifa iliyotangazwa leo na Kocha Mkuu, Oscar Milambo, kimehusisha jumla ya wachezaji 23, ambapo kitaingia kambini Jumapili hii hadi Novemba 16 mwaka huu.