LIGI ya vijana chini ya umri wa miaka 15 ya Azam (Azam Youth League U-15) imeendelea wikiendi iliyopita kwa mechi tatu kupigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Timu ngeni ya Tanzanite iliyochukua nafasi ya New Talent iliyokiuka sheria za michuano hiyo, iliweza kuanza vibaya baada ya kuchapwa mabao 3-1 na JMK Park katika mechi ya awali.

Bom Bom iliyoanza kwa kipigo kwenye wiki ya kwanza, iliweza kujirekebisha kwa kuichapa Florida mabao 8-1.

Wenyeji Azam U-15 walifanikiwa kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Rendis katika mchezo uliofunga dimba Jumamosi ya wikiendi iliyopita.

Wakati michuano hiyo ikimaliza wiki ya pili ikifanyika kila Jumamosi ya wiki kwa muda wa wiki 10, msimamo unaonyesha kuwa JMK Park iko kileleni kwa pointi sita, ikifuatiwa na Azam yenye pointi nne sawa na Rendis katika nafasi ya tatu.

Bom Bom imejikita katika nafasi ya nne ikiwa na pointi tatu huku Florida na Tanzania zikifunga dimba kwenye nafasi ya tano na sita zikiwa hazivuna pointi zozote.