KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, sasa inakupa fursa shabiki wa timu hiyo ya kuwatunuku wachezaji wako pendwa kila mwezi wakati wa mechi za mashindano.

Tuzo hizo ni maalumu kabisa inayodhaminiwa na Benki ya NMB ambao ni wadhamini wetu wakuu, inayokwenda kwa jina la ‘NMB Player of the Month’, ambayo itatolewa kila mwezi kwa mchezaji bora aliyefanya vizuri kwa mwezi husika.

Kwa kuanza rasmi mchakato, wakati Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ikiwa imeanza rasmi Agosti 26 kwa Azam FC kuichapa Ndanda bao 1-0, sasa tunakupa fursa ya kumchagua mchezaji bora wa mwezi huo uliopita.

Tuzo hiyo ya kwanza itatolewa wiki ijayo Septemba 23 mwaka huu, kabla ya kuanza mchezo wetu ujao wa ligi dhidi ya Lipuli utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, kuanzia saa 1.00 usiku.

Azam B nao kuhusika

Ujio wa tuzo hizo haujawaacha mbali timu ya vijana ya Azam FC (Azam FC U-20), kwani nao watatunukiwa kila mwezi kama ilivyo kwa timu kubwa.

Tuzo za Azam B zinadhaminiwa na wadhamini wetu wengine maji safi ya Uhai Drinking Water yanayokata kiu yako na kuondoa uchovu kutoka Bakhresa Food Products, tuzo hiyo itaitwa ‘Uhai Player of the Month.

#TimuBoraBidhaaBora