WINGA wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Joseph Kimwaga, aliyefanyiwa upasuaji wa goti nchini Afrika Kusini hivi karibuni tayari amerejea nchini jana

Kimwaga ameishukuru mno Bodi ya Wakurugenzi ya timu hiyo kwa moyo wa huruma waliokuwa nao na sapoti wanayotoa kwa wachezaji na hiyo ni kutokana na mpango mzuri waliokuwa nao wa kuwafanyia matibabu wachezaji nje ya nchi pale wanapatwa na matatizo makubwa ya kiafya.

“Ni suala la kuishukuru timu na bodi kwa ujumla kwa sababu sio kitu kidogo ni jambo la gharama, lakini tunashukuru kwa sapoti wanayotupatia wachezaji na moyo wa huruma waliokuwa nao kwa sababu kiukweli ni gharama sio kitu rahisi, ila tunashukuru sana kwa kitu wanachofanya kwani ni njia ya kiprofesheno zaidi kama wenzetu walioendelea ni vitu vya kawaida,” alisema Kimwaga wakati azkizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz

Kimwaga alisema kwa mazingira ya Tanzania vitu kama hivyo ni adimu, akidai kuwa hata kwa upande wao wachezaji ni mambo mageni kwao.

“Wachezaji wengi wakifanyiwa vitu kama hivi huwaga anahisi kwamba labda ndoto zake ndio zishapotea, lakini mimi binafsi naamini hapa nishatibu tatizo limekaa vizuri, ni kujipanga upya tu nikirudi, naimani nitarudi tu vizuri sana kikubwa katika moyo wangu na nitaendelea kupambana,” alisema.

Winga huyo ambaye amepitia kwenye mpango wa kukuza vipaji wa kituo cha Azam Academy, anatarajia kukaa nje ya dimba kwa muda wa miezi mine kutibu tatizo lake hilo la goti, akiumia mtulinga wa kati (meniscus) wa eneo hilo.