KWA niaba ya Uongozi na Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, tunawapongeza viongozi wote wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), waliochaguliwa kwenye Mkutano Mkuu wa Uchaguzi uliofanyika mkoani Dodoma leo.

Pongezi zaidi ziende kwa Rais mpya wa TFF, Wallace Karia na Makamu wake, Michael Wambura. Tunapenda kuwapa hongera na kuwatakia kheri kwenye uongozi wao kwa kipindi chote watakachohudumu.

Tunaamini kupitia kwao na wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa, mpira wetu utazidi kupiga hatua.

Ukawe uongozi utakaozingatia uweledi na uadilifu.

#TimuBoraBidhaaBora