KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, sasa imeongezewa mechi moja ya kirafiki jijini Kampala, Uganda baada ya Vipers kuthibitisha kucheza nayo Agosti 11 mwaka huu.

 

Tayari mechi nyingine tatu zimeshathibitishwa, ambapo Azam FC itaanza kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya KCCA Alhamisi ijayo saa 10.00 jioni, ukifuatiwa na huo wa Vipers, itachuana na Ondurapaka Agosti 13 kabla ya kuhitimisha ziara kwa kukipiga na URA Agosti 14.