KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inatarajia kuanza rasmi mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao kwa kuanzia ugenini ikivaana na Ndanda katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara Agosti 26, mwaka huu.

Pazia hilo la ligi litafunguliwa kwa mechi ya Ngao ya Jamii, baina ya Yanga waliokuwa mabingwa wa ligi msimu uliopita na mabingwa wa Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC), Simba, utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Agosti 23 mwaka huu.

Mara baada ya kukipiga na Ndanda, Azam FC itarejea jijini Dar es Salaam kucheza mchezo wa pili ambao ni dhidi ya Simba, uliopangwa kufanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Septemba 2 mwaka huu, kabla ya kukipiga na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex Septemba 9.

Azam FC itamaliza mechi tano za mwanzo kwa mechi mbili zingine nyumbani, ambapo itamenyana na Lipuli Septemba 17 mwaka huu na kisha kuikabili Singida United Septemba 23 mwaka huu, timu zote hizo mbili zikiwa zimetoka kupanda daraja msimu huu.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, inaonyesha kuwa Azam FC itacheza jumla ya mechi sita nyumbani na tisa ugenini katika mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo huku raundi ya pili ikicheza sita ugenini na tisa nyumbani

Ratiba kamili Azam FC Ligi Kuu (2017-2018):

*26.08.2017 (Sat) – Ndanda vs Azam FC – Nangwanda Sijaona – 16.00HRS

*02.09.2017 (Sat) – Azam FC vs Simba SC – National Stadium (Dar) – 19.00HRS

*09.09.2017 (Sat) – Azam FC vs Kagera Sugar – Azam Complex (Dar) – 19.00HRS

*17.09.2017 (Sun) – Azam FC vs Lipuli – Azam Complex (Dar) – 19.00HRS

*23.09.2017 (Sat) – Azam FC vs Singida United – Azam Complex (Dar) – 19.00HRS

*01.10.2017 (Sun) – Mwadui FC vs Azam FC – Mwadui Complex (Shinyanga) – 16.00HRS

*07.10.2017 (Sat) – Mbao FC vs Azam FC – CCM Kirumba Stadium (Mwanza) – 16.00HRS

*15.10.2017 (Sun) – Mbeya City vs Azam FC – Sokoine Stadium (Mbeya) – 16.00HRS

*21.10.2017 (Sat) – Azam FC vs Ruvu Shooting – Azam Complex (Dar) – 19.00HRS

* 30.10.2017 (Mon) – Azam FC vs Njombe Mji – Azam Complex – 19.00HRS

*06.11.2017 (Mon) – Azam FC vs Mtibwa Sugar – Azam Complex – 19.00HRS

*11.11.2017 (Sat) – Stand United vs Azam FC – Kambarage Stadium – 16.00 HRS

*20.11.2017 (Mon) – Majimaji vs Azam FC – Majimaji Stadium – 16.00HRS

*15.12.2017 (Fri) – Tanzania Prisons vs Azam FC – Sokoine Stadium – 16.00HRS

* 23.12.2017 (Sat) – Yanga SC vs Azam FC – National Stadium – 16.00HRS

* 29.12.2017 (Fri) – Azam FC vs Ndanda – Azam Complex – 19.00HRS

*20.01.2018 (Sat) – Simba SC vs Azam FC – National Stadium – 1600HRS

* 27.01.2018 (Sat) – Kagera Sugar vs Azam FC – Kaitaba Stadium – 16.00HRS

*02.02.2018 (Fri) – Lipuli FC vs Azam FC – Samora Stadium – 16.00HRS

*12.02.2018 (Mon) – Singida United vs Azam FC – Namfua Stadium – 16.00HRS

*19.02.2018 (Mon) – Azam FC vs Mwadui – Azam Complex – 19.00HRS

* 24.02.2018 (Sat) – Azam FC vs Mbao FC – Azam Complex – 19.00HRS

*04.03.2018 (Sun) – Azam FC vs Mbeya City – Azam Complex – 19.00HRS

*10.03.2018 (Sat) – Ruvu Shooting vs Azam FC – 16.00HRS

*17.03.2018 (Sat) – Njombe Mji vs Azam FC – Sabasaba Stadium – 16.00HRS

*31.03.2018 (Sat) – Mtibwa Sugar vs Azam FC – Manungu Stadium – 16.00HRS

*06.04.2018 (Fri) – Azam FC vs Stand United – Azam Complex – 19.00HRS

*4.04.2018 (Sat) – Azam FC vs Majimaji – Azam Complex – 19.00HRS

*28.04.2018 (Sat) – Azam FC vs Tanzania Prisons – Azam Complex – 19.00HRS

*05.05.2018 (Sat) – Azam FC vs Yanga SC – National Stadium – 16.00HRS