KIKOSI cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, kimewasili salama jijini KIgali, Rwanda usiku wa kuamkia leo, tayari kabisa kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wao Rayon Sports.

Safari ya kikosi hicho imechukua takribani siku mbili, ambapo itamenyana na mabingwa hao wa Rwanda kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Nyamirambo saa 10.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Azam FC imefikia katika Hoteli ya Hilltop iliyopo jijini hapa, ambapo kwa mujibu wa programu ya benchi la ufundi, kikosi hicho kitafanya mazoezi leo jioni muda utakaopigwa mchezo huo.

Rayon Sports itautumia mchezo huo kama sehemu maalumu ya kusheherekea ubingwa wao wa ligi walioutwaa msimu huu.