KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inasikitika kutangaza kifo cha baba mzazi wa kiungo wa timu hiyo Frank Domayo, anayejulikana kama Raymond Domayo, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kuugua ghafla.

Uongozi wa Azam FC unachukua fursa hii kutuma salamu za rambirambi kwa familia ya Domayo kutokana na pigo hilo na itaendelea kuwa pamoja na mchezaji wetu huyo katika kipindi hiki kigumu pamoja na ndugu jamaa na marafiki walioguswa moja kwa moja na msiba huo.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa familia hiyo, msiba upo nyumbani kwa kiungo huyo Tabata Kisiwani.

Katika kuonyesha umoja wa kumsapoti mchezaji wetu, kikosi cha Azam FC ambacho hivi sasa kipo safarini kutokea mkoani Tanga kilipoenda kucheza na JKT Ruvu, msafara wote utapitia nyumbani kwa kiungo huyo kwenda kutoa pole kwa familia

Inna Lillahi Wa inna Ilayhi Raji’un

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe. Amen!