TIMU ya Azam Veteran jioni ya leo imeiangamiza Football Fans mabao 6-3 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Huo ni mwendelezo wa mechi za kirafiki wa timu hiyo kwa wachezaji kujiweka sawa kiafya ikiwemo kujiandaa na michuano mbalimbali inayotarajia kushiriki hapo baadaye.

Mabao ya Azam Veteran yamefungwa na mshambuliaji hatari wa timu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’, aliyefunga peke yake mabao matatu ‘hat trick’, huku Mwenyekiti wa Azam FC, Nassor Idrissa ‘Father’, ambaye ni kiungo nyota wa timu hiyo akifunga bonge la bao kwa shuti la kiufundi nje ya eneo la 18.

Wengine waliofumania nyavu za Football Fans, ni Awadh Afif na Abdallah Kajembe, waliofunga moja kila mmoja na kuhitimisha ushindi huo mnono.