KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inapenda kutuma salamu za rambirambi kwa uongozi wa klabu ya Kagera Sugar baada ya kufariki dunia kwa kipa wao, David Buruani, usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, Buruani amekutwa na umauti ghafla katika Hospitali ya Bugando mkoani Mwanza baada ya kuugua ghafla.

Azam FC inaungana na klabu hiyo, wanafamilia, wapenzi wa soka, ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza kifo hicho cha kuondokewa na mpendwa wao na tunawaomba wawe na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.

Inna Lillahi wa Inna Ilaihi Raji’un.