KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inatarajia kuanza rasmi kampeni ya kuwania taji la michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) kwa kukipiga na Cosmo Politan.

Mchezo wa raundi ya tano ya michuano hiyo, unatarajia kufanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Jumatatu ijayo (Januari 23).

Azam FC inarejea tena kwenye kivumbi cha michuano hiyo msimu huu, ikiwa na kumbukumbu ya kufika fainali msimu uliopita lakini ikapoteza kwa kufungwa mabao 3-0 na Yanga.

Pia ilishuhudiwa kipa wake namba moja, Aishi Manula, akichaguliwa kuwa Kipa Bora wa michuano hiyo.

Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi, wamejidhatiti vilivyo kulitwaa taji hilo msimu huu kufuatia kujiwekea malengo ya kufanya hivyo hasa ikizingatiwa bingwa wa michuano hiyo atakata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.

Tayari Azam FC imeshakata tiketi ya kushiriki michuano hiyo mwaka huu, ambapo ratiba inaonyesha kuwa itaanzia raundi ya kwanza kwa kucheza na mshindi wa jumla ya mchezo wa raundi ya awali kati ya Orapa United ya Botswana na Mbabane Swallows ya Swaziland.

Bocco arudi nyumbani

Nahodha wa Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’, kwa mara ya kwanza mchezo huo wa FA Cup utamfanya arejee Cosmo Politan, ambayo ndiyo timu yake ya zamani aliyokulia kabla ya matajiri hao kumsajili kutoka hapo miaka nane iliyopita.

Hivyo itakuwa ni historia nzuri kwa Bocco siku hiyo, ambaye atakuwa na kazi moja tu ya kuiongoza Azam FC kuhakikisha inasonga mbele kwa raundi ya sita ya michuano hiyo kwa kuitoa timu yake hiyo, ambayo kwa sasa inashiriki Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara (SDL).

Mechi zingine

Ukiondoa mtanange huo, ratiba ya mechi nyingine za raundi hiyo ipo kama ifuatavyo;

Januari 21, 2017

Alliance v Mbao (CCM Kirumba, Mwanza)

Majimaji v Mighty (Majimaji, Ruvuma)

Yanga v Ashanti United (Uhuru, Dar es Salaam)

January 22, 2017

Ruvu Shooting v Kiluvya United (Mabatini, Pwani)

Toto African v Mwadui (CCM Kirumba, Mwanza)

Simba SC v Polisi Dar (Uhuru, Dar es Salaam)

Mbeya Warriors v Tanzania Prisons (Sokoine, Mbeya)

Polisi Mara v Stand United (Karume, Musoma)

Ndanda v Mlale JKT (Nangwanda Sijaona, Mtwara)

January 24, 2017

Polisi Moro v Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro)

Kurugenzi FC v JKT Ruvu (Mafinga, Iringa)

Mbeya City v Kabela City (Sokoine, Mbeya)

Madini FC v Panone FC (Sheikh Amri Abeid, Arusha)

January 25, 2017

Singida United v Kagera Sugar (Namfua, Singida)

TBA

African Lyon v Mshikamano (Uhuru, Dar es Salaam).