KITUO cha kukuza vipaji cha nchini Kenya cha Green Sports Africa, tayari kipo nchini kwa ziara ya siku tano itakayoambatana na michezo mbalimbali ya kirafiki zikihusisha timu zao za vijana.

Azam FC ambayo ndio wenyeji wao wanatarajia kucheza nao mechi mbili za kirafiki zitakakazofanyika keshokutwa Jumamosi, ikianza kukipiga na timu maalum ya vijana chini ya umri wa miaka 17 iliyopo kwenye programu ya jamii ya Azam FC, itakayoanza saa 10.00 jioni.

Timu ya vijana ya Azam FC chini ya umri wa miaka 21, nayo itajitupa uwanjani saa 12.00 jioni siku hiyo kukipiga na vijana wa umri huo wa Green Sports.

Mechi nyingine

Mbali na mechi hizo, pia Azam FC imeiandalia mechi nyingine Green Sports, ambapo leo sa 11.00 jioni n saa 12.30 timu yao chini ya umri wa miaka 13 na 16, itaumana na timu za umri huo za kituo cha JMK Academy, mechi zote zikifanyika Uwanja wa JMK.

Mechi nyingine zitafanyika kesho Ijumaa, timu yao chini ya umri wa miaka 17 itakipiga dhidi ya JAKI Academy ya Mbagala saa 10.00 jioni kabla ya Green Sports U-21 kuivaa Udizungwa FC saa 12.00 jioni.