KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, imefanya mabadiliko kidogo kuhusu mpango wake wa Kitaifa wa kusaka wachezaji wenye umri wa miaka 17 (U-17), ambapo badala ya kwenda Visiwani Zanzibar Oktoba 8 mwaka huu, sasa zoezi hilo limehamishiwa mjini Tanga tarehe hiyo.

Kuahirishwa kwa zoezi hilo Visiwani Zanzibar kunatokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu hasa baada ya Uwanja wa Amaan, Zanzibar tuliopanga kufanyia majaribio hayo kuwa na matumizi mengine siku hiyo, kwa tarehe nyingine ya majaribio kwa wakazi wa Zanzibar (Unguja na Pemba) tunatarajia kupanga hivi karibuni.

Hivyo, kama umezaliwa kuanzia mwaka 2000, 2001 na 2002 na unaishi mkoani Tanga, unaombwa kufika na kuonyesha kipaji chako kwenye majaribio ya nne ya wazi kuendeshwa na Azam FC yatakayofanyika Uwanja wa Mkwakwani Jumamosi ya Oktoba 8, 2016.

Tafadhali unaombwa kufika na nakala ya cheti chako cha kuzaliwa kwa wale wote watakaokuja kwenye majaribio hayo.

Awali zoezi hilo lilimalizika kwa mafanikio makubwa sana mkoa wa Dar es Salaam katika Wilaya za Temeke, Kigamboni, Ilala, Kinondoni na kwa Azam FC kuvuna jumla ya vipaji 15 wataoingia kwenye fainali ya mwisho ya mikoa yote Novemba mwaka huu.

Kwa majaribio mengine ya wazi kuhusu sehemu, tarehe na muda, tutawatangazia hivi karibuni.

Tafadhali washirikishe ujumbe huu rafiki zako!