NYOTA wanne wa timu ya vijana ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC ‘Azam FC Academy’, wameula kwenye kikosi bora cha michuano ya vijana ya Afrika Mashariki ‘Azam Youth Cup 2016’ iliyomalizika jana usiku.

Michuano hiyo iliyoandaliwa na Azam FC na kufanyika ndani ya Uwanja wa Azam Complex, Chamazi ikishirikisha timu nne (Azam Academy, Ligi Ndogo Academy-Kenya, Football for Good Academy- Uganda na Future Stars Academy- Arusha), ilishuhudiwa Azam ikiibuka mabingwa.

Wachezaji wa mabingwa hao walioula kwenye kikosi hicho kilichochaguliwa na jopo la makocha walioshuhudia michuano hiyo ni beki bora Abbas Kapombe, kiungo Prosper Mushi, Rajab Odas, mfungaji bora na mshambuliaji bora, Shaaban Idd.

Kikosi bora cha michuano kinaundwa;

 1. Rogers Siteti- Ligi Ndogo
 2. Justin Opiro- Football for Good
 3. Geoffrey Cancura- Football for Good
 4. Abbas Kapombe- Azam Academy   
 5. Rogers Atube- Football for Good
 6. Allan Ganukura- Football for Good
 7. Stephen Bongomin- Football for Good
 8. Prosper Mushi- Azam Academy
 9. Shaaban Idd- Azam Academy
 10. Rajab Odas– Azam Academy
 11. Solomon Mbiti- Ligi Ndogo Academy

                         #AzamYouthCup2016