KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imepangwa kucheza na Ashanti United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara kwenye mchezo wa raundi ya tatu wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup).

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo, imeonyesha kuwa raundi hiyo inatarajiwa kuendelea kuanzia Januari 12 na wikiendi ya Januari 23 hadi 27 mwaka huu, kwa timu 32 kuchuana kuwania kufuzu kwa hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Azam FC ambao ndio vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) wakiwa na pointi 35, watapambana na Ashanti United katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam Januari 26 mwaka huu.

Matajiri hao kutoka viunga vya Azam Complex moja ya vituo bora vya soka barani Afrika, watakuwa wakicheza kwa mara ya kwanza michuano hiyo iliyofufuliwa msimu huu, tokea ipande daraja la Ligi Kuu mwaka 2008.

Azam FC imeungana na timu nyingine 15 za  Ligi Kuu kuingia moja kwa moja kwenye raundi hiyo, ambazo zimeunana na nyingine 16 zilizofuzu kutoka raundi ya pili yenye timu kutoka Ligi Daraja la Kwanza (FDL)na Ligi Daraja la Pili (SDL).

Mabingwa hao wa Kombe la Kagame, wamepania vilivyo kutwaa ubingwa wa michuano hiyo, ili kujiwekea mazingira ya kuandika rekodi ya kulibeba taji hilo kwa mara ya kwanza na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.

Mechi nyingine raundi ya tatu;

Januari 12, 2016

Majimaji v JKT Mlale

(Uwanja wa Majimaji, Songea)

Januari 23, 2016

Pamba v Toto Africans

(Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza)

Ndanda FC v Mshikamano

(Uwanja wa Nagwanda Sijaona Mtwara)

Burkinafaso v Simba SC

(Uwanja wa Jamhuri, Morogoro)

Januari 24, 2016

Yanga v Friends Rangers

(Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)

Njombe Mji v Tanzania Prisons

(Uwanja wa Amani, Shinyanga)

Stand United v Mwadui FC.

(Uwanja wa Kambarage, Shinyanga)

Januari 25, 2016

Kagera Sugar v Rhino Rangers

(Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora)

Panone v Madini

(Uwanja wa Ushirika, Moshi)

Januari 26, 2016

Mtibwa Sugar v Abajalo

(Uwanja wa Jamuhuri, Morogoro)

Lipuli/Kurugenzi v JKT Ruvu

(Uwanja wa Wambi, Mafinga)

African Sports v Coastal Union

(Uwanja wa Mkwakwani, Tanga)

Geita Gold v Mgambo JKT

(Uwanja wa Nyankungu, Geita)

Januari 27, 2016

Singida United v Mvuvumwa

(Uwanja wa Namfua, Singida)

Wenda v Mbeya City

(Uwanja wa Sokoine, Mbeya)