TIMU ya Azam Veteran juzi jioni ilifanya mambo makubwa baada ya kuwatandika maveterani wenzao kutoka Kigamboni mabao 7-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Kikosi cha Azam Veteran kinaundwa na baadhi ya viongozi wa timu ya Azam FC kama vile Makamu Mwenyekiti Idrissa Nassor ‘Father’ anayependelea kucheza eneo la kiungo na Meneja wa timu, Luckson Kakolaki katika sehemu ya ulinzi.

Mchezo huo wa kirafiki uliofanyika siku ya kumbukumbu ya Uhuru wa Tanzania Bara, ulishuhudia Azam Veteran ikitawala sehemu kubwa ya mchezo huo.

Mabao ya Azam Veteran kwenye mchezo huo yalifungwa na winga wa Azam FC, Kelvin Friday, aliyefunga mawili, Abdul Karim, Kelvin, Salim walifunga moja kila mmoja katika kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Azam Veteran iliendelea kushusha mvua nyingine ya mabao kwa kupachika mengine manne kupitia kwa Kantona, Abdallah, Salim likiwa ni bao lake la pili kwenye mchezo huo pamoja na  Seleman.