Kikosi cha timu ya Azam FC leo saa 10 jioni kitafanya mazoezi yake ya kwanza mkoani Mtwara kabla ya kuivaa Ndanda FC kesho,

Wachezaji waliopo na timu mkoani Mtwara wapo katika hali nzuri na wamehamasika kuondoka na pointi tatu muhimu mkoani Mtwara mara baada ya kikao kifupi na benchi la ufundi cha kuwekana sawa kilichofanyika mara baada ya mazoezi ya jana Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam kabla ya kuondoka.