Wachezaji Kipre Bolou na Khamis Mcha Viali wa Unguja wameanza mazoezi na kikosi cha kwanza baada ya kuwa nje ya kikosi kwa muda mrefu kutokana na majeraha.

 

Bolou aliyefanyiwa matibabu nchini Afrika ya Kusini alicheza kwa dakika 45 kwenye kikosi cha Under 20 na sasa ameanza mazoezi na kikosi cha kwanza kwa 100%. Hali kadhalika Mcha naye ameungana na kikosi cha kwanza cha Azam FC hii leo baada ya kumaliza program ya matibabu na mkuu wa idara ya tiba ya viungo.

 

Upande wa mlinzi Racine Diof, baada ya kuwa nje ya uwanja kwa siku tano baada ya kupata majeraha kwenye mechi dhidi ya Coastal Union, beki huyo toka Afrika Magharibi leo amefanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Azam FC.

 

Mchezaji pekee ambaye bado anajiuguza ni Waziri Salum ambaye bado anaendelea na program ya matibabu.

 

Azam FC imeendelea na mazoezi chini ya waalimu wasaidizi Mario na Kitambi kutokana na kocha mkuu Stewart Hall kuwa safarini nchini Dubai kwa mapumziko ya wiki moja ambapo atarejea nchini keshokutwa alhamisi.

 

Azam FC inajiandaa kwa mchezo dhidi ya Yanga utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam taree 17/10/2015