Kamati ya uendeshaji ligi ya TPLB  imemfungia nahodha wa MCCA Juma Said Nyoso wa Mbeya City kwa miaka miwili na kumtoza faini ya Sh Milioni 2, kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia Nahodha wa Azam FC John Raphael Bocco.

Nyoso alifanya kitendo hicho katika kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, hiyo ikiwa mara ya nne na mara pili kwa mwaka kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu kwenye michezo ya Ligi Kuu.

Ni matarajio yetu kuwa MCCA watamuongoza Nyosso kwenda mbele ya vyombo vya habari kumuomba msamaha John Bocco, Azam FC na wapenda soka nchini na kitendo kile ambacho kinatia doa na kurudisha nyuma juhudi za kujenga soka la Tanzania