Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam leo umeiwezesha Azam FC kufikisha mechi tano bila kupoteza wala kutoka sare.

Mchezo huo uliocheeshwa na refa Alex Mahagi wa Mwanza, mabao ya Azam FC yalifungwa na Shomari Kapombe na mshambuliaji Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast, yote kipindi cha pili.

 

 

Kapombe alifunga bao safi dakika ya 47 akimalizia mpira wa kona uliopigwa na winga Farid Mussa, wakati Kipre Tchetche alifunga dakika ya 74 akimalizia krosi ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy.

Kikois cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Racine Diouf, Pascal Wawa, Said Mourad, Farid Mussa, Frank Domayo, Jean Baptiste Mugiraneza, Ramadhani Singano ‘Messi’/Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dk65, Allan Wanga/Didier Kavumbangu dk72 na Kipre Tchetche/Ame Ali ‘Zungu’ dk77.

Coastal Union; Sebwato Nicholas, Hamad Juma, Tumba Lui, Yassin Mustafa, Abdallah Mfuko, Youssoufa Sabo, Twaha Ibrahim ‘Messi’, Nassor Kapama/Mohammed Hamisi dk56, Ali Ahmed ‘Shiboli’/Chidiebele Abasalim dk61, Ayoub Yahaya na Ismail Mohammed.