Azam FC inaweza kukaa kileleni leo endapo itaifunga Coastal Union ya Tanga huku Mtibwa na Yanga zikitoka sare.

 

Historia inatuambia kuwa Yanga wamekuwa na wakati mgumu sana wanapokabiliana na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri mji kasoro bahari “Mlogolo” Morogoro na hili linaweza kujitokeza tena leo na kuipa chance Azam FC ya kukaa kileleni.

 

Endapo Azam FC itashinda leo, basi itakuwa inashinda mchezo wa tato mfululizo na kuweka rekodi yake binafsi kwenye ligi kuu.

 

Azam FC iliyo chini ya Stewart John Hall, itaendelea kuwakosa nyota wake Kipre Bolou na Khamis Mcha “Viali” walio majeruhi huku Aggrey Morris akimalizia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata Mwadui Shinyanga.

 

Kwa mujibu wa ratiba ya kituo cha kurusha matangazo ya ligi kuu cha Azam TV. Mchezo kati ya Azam FC na Coastal Union utarushwa live na ZBC2.

 

Mtandao huu unaitakia kila la kheri Azam FC