Kikosi cha Azam FC kimetua kwenye viunga vya uzunguni vya mgodi wa dhahabu wa Mwadui kabla ya kukabiliana na watoto wa Jamhuri Kihwelu aka Talantin Alberto Pereira hapo kesho.

Ulimwengu wa soka nchini unajua ufundi, ushindani, majigambo na uzoefu wa Julio kwenye soka la Tanzania ambao utakuwa ukichagizwa na wachezaji wazoefu aliowasajili kama Jabir Aziz Stima, Nizar Khalfan, Paul Nonga na wengineo.

Lakini Azam FC ipo imara na kama inavyojulikana msimu huu tangia mashindano ya CECAFA Kagame Cup, Azam FC haijapoteza mchezo hata mmoja wa mashindano huku ikiruhusu bao moja tuu kutinga kwenye vyavu zake.

Azam FC hapo kesho itawategemea sana nyota wake Allan Wanga, Kipre Tchetche, John Bocco, Farid Mussa, na Didier Kavumbagu kuweza kupata magoli ya kutosha na kujikusanyia pointi tatu muhimu sana.

Mechi ya kesho ya Azam FC itarushwa moja kwa moja na Azam TV