Baada Azam FC kuichapa Tanzania Prisons 2-1 kocha mkuu , Muingereza Stewart Hall amesema, kipigo hicho ni mwanzo tu na mpango wake ni kuchapa timu zote zinazokuja mbele yetu.

 

Azam FC ambayo Jumatano hii itakuwa ugenini Shinyanga kuivaa Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage, ilifungua pazia la Ligi Kuu Bara kwa ushindi huo huku ikiwakosa wachezaji wa kikosi cha kwanza ambao ni John Bocco ‘Adebayor’, Shomary Kapombe, Msenegal Rasine Diof ambao ni majeruhi.

 

Kocha  Stewart amesema, anataka timu ishinde kwa mabao mengi kutokana na ubora wa wachezaji alionao hasa kwenye safu ya ushambuliaji ambao ni Mrundi Didier Kavumbagu, Mkenya Allan Wanga, Muivory Coast Kipre Tchetche, Ame Ally, Bocco, Mcha Hamis, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Farid Mussa lakini wanamwangusha.

 

“Tumeshinda lakini tunahitaji kushinda kwa idadi kubwa mabao, kuwa na washambuliaji kama Kavumbagu, Wanga, Tchetche, Bocco, Ame na Messi tunakila sababu ya kushinda tu,”alisema Stewart.

 

“Katika mechi yetu na Prisons tungeshinda zaidi ya mabao manne au matano lakini  washambuliaji walipoteza nafasi nyingi, hata hivyo, katika kipindi hiki tutawekana sana kuhakikisha tunakamilisha malengo yetu.”

 

Hata hivyo, ishindi huo, unaifanya Azam FC kukaa kileleni mwa ligi nyuma ya Yanga kwa tofauti ya goli moja baada ya kuifunga Coastal Union ya Tanga jioni hii magoli 2-1.